Mkapa Awataka WanaCCM Wavunje Makundi......Asema Mtu Anayehama Chama ni Msaliti na Hafai kuwa Kiongozi


RAIS mstaafu Benjamin Mkapa amewaasa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuacha kambi ambazo ziliweza kusababisha majimbo mawili kuchukuliwa na Chama cha Wananchi (CUF) mkoani Lindi katika uchaguzi wa mwaka 2010.

Rais Mkapa aliyasema hayo jana wakati alipokuwa akizungumza na wanachama wa chama hicho katika mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi ya Mpilipili mjini Lindi.

Alisema “acheni tabia hiyo kwani mchakato wa kumpata mgombea inakuwa na utaratibu wake na inapotekelezwa anapatikana mmoja ili apeperushe bendera ya chama”.

Mkapa alisema wale wote ambao walishiriki kwenye kura za maoni za kumtafuta mgombea ubunge, wanatakiwa kuwa wamoja wakishirikiana na yule aliyeteuliwa kuhakikisha chama kinashinda katika uchaguzi wa mwaka huu.

Alisema kwenye uchaguzi wa Oktoba 25, mwaka huu tabia hiyo iachwe mara moja ili ushindi uwe wa CCM. Alisema mgombea anaposhindwa kwenye michakato hiyo ndiyo anasema mfumo mbaya wakati wote yeye alikuwapo mwanzo mpaka mwisho, akishashindwa anaamua kulalamika na kuhama chama.

Alimtaja mtu wa aina hiyo kuwa ni msaliti wa chama na hafai kuwa kiongozi. 
 
Kiongozi huyo mstaafu alisema mawaziri watatu waliokaa zaidi ya miaka 15 kwenye serikali ya CCM kuanzia uwaziri hadi uwaziri mkuu na kuondoka wakidai serikali hiyo haifai, wao ndio hawafai kuongoza nchi
Share on Google Plus

    Blogger Comment