Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli ameombwa kuwafuta kazi baadhi ya viongozi wa chama hicho ambao wamebainika kuwa wanakihujumu kwa kumsaidia mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa.
Katika
hali inayoonesha kuwa kuna mchwa wanaokitafuna kwa kificho chama hicho,
mjumbe wa kamati ya kampeni ya CCM mkoani Arusha, Victor Njau alimuomba
Dk. John Magufuli kuwafukuza kazi mara moja watendaji ambao
wanakihujumu chama hicho katika harakati hizi za kampeni.
“Kuna
viongozi wanatumia magari ya CCM, wanalipwa mishahara lakini
wanaendesha kampeni za kuwaangusha wagombea wa chama tawala. Tunamtaka
Dk. Magufuli akishinda aanze na wasaliti hawa,” alisema.
Hii
inaonesha kuwa viongozi wanaodaiwa kukisaliti chama hicho wanafahamika
na tayari ‘faili’ lao limewekwa sawa wakisubiri adhabu yao mara tu baada
ya Dk. Magufuli kuingia ikulu, endapo atachaguliwa na wananchi Oktoba
25, mwaka huu.
Hili
sio suala geni kwa mgombea huyo wa urais kwani alishawahi kuweka wazi
kuwa anawafahamu baadhi ya watu wanawasaliti kwa kumsaidia mgombea wa
Chadema, Edward Lowassa. Aliwakanya watu hao na kuahidi kuwawajibisha
pindi atakapoingia madarakani, la sivyo waache usaliti huo
Blogger Comment