Mwili wa Mhe. Celina Kombani waagwa viwanja vya Karimjee, Dr. Bilali aongoza wananchi kuomboleza


HALI ya huzuni imetawala wakati wa kuagwa kwa aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani.

Mwili wa Kombani umeagwa rasmi leo katika Uwanja wa Karimjee jijini Dar es Salaam tayari kwa ajili ya mazishi kesho mkoani Morogoro.

Watumishi wa serikali, wana familia ya Kombani na wananchi kwa ujumla walibubujikwa na machozi wakati wasifu wa kiongozi huyo wa nchi ukitolewa.

Celina Kombani ambaye amekuwa mbunge kwa miaka 10 katika Jimbo la Ulanga Mashariki, mkoani Morogoro alifariki dunia Septemba 23, 2015 katika Hospitali ya Apolo, India alipokwenda kwa matibabu ya maradhi ya Saratani yaliyokuwa yakimsumbua kwa muda mrefu.

Baadhi ya viongozi waliohudhuria tukio hilo ni pamoja na Makamu wa Rais, Gharib Bilal; Spika wa Bunge, Anna Makinda; Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue; Makamu Mwenyekiti wa CCM- Bara, Philip Mangula; Mama Maria Nyerere, Jaji Joseph Warioba pamoja na mawaziri na wabunge wanaomaliza muda wao.

Salamu za pole zilitolewa kutoka kwa watu mbalimbali. Salamu kutoka CCM zilitolewa na Zakia Meghi ambaye amesema, amekuwa akishiriki katika uandaaji wa Ilani ya uchaguzi ya chama hicho pamoja na kukitumikia katika nyadhifa mbalimbali.

Kwa niaba ya umoja wa wabunge wanawake salamu zilitolewa na Angela Kairuki huku Spika Makinda akitoa salamu kwa niaba ya Bunge huku Makamu wa Pili wa Rais, Zanzibar Seif Idd akitoa salamu za pole kwa niaba ya Serikali ya SMZ.

Kombani alizaliwa Juni 19, 1959 huku akipata elimu yake ya msingi katika Shule ya Msingi Kwiro (1975), elimu ya sekondari katika shule ya Kilakala (1978) na ya Kidato cha Tano na Sita katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Tabora (1981).

Kombani alisoma katika Chuo Kikuu cha Mzumbe, Morogoro akibobea katika Utawala wa Umma. Alitunukiwa shahada ya kwanza mwaka 1985 na baadaye shahada ya uzamili 1995.

Baadhi ya nafasi ambazo Kombani aliwahi kuzishika ndani ya CCM ni uenyekiti wa Umoja Wanawake (UWT) Wilaya ya Morogoro (2002-2005), Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji CCM Wilaya ya Kilosa (1987-1992).

Kwa upande wa serikali, Kombani aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI (2006-2008) kabla ya kupandishwa ngazi na kuwa waziri kamili wa wizara hiyo hiyo mwaka (2008-2010).

Baada ya uchaguzi mkuu 2010 Kombani huyu aliteuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria kabla ya kubadlisha ofisi hiyo mwaka 2014 na kuwa Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti na Utumishi wa Umma, nafasi ambayo aliitumikia mpaka mauti yalipomkuta.
Name:  3.png
Views: 671
Size:  369.0 KB
Name:  2.png
Views: 664
Size:  391.5 KBViongozi waandamizi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania


Name:  4.png
Views: 669
Size:  379.9 KBMakamu wa Rais Dr. Bilal akitoa heshima za Mwisho


Name:  7.png
Views: 648
Size:  411.5 KBMama wa Taifa Mama Maria Nyerere akitoa heshima za Mwisho
Name:  5.png
Views: 636
Size:  341.4 KBMke wa Rais wa JMT Mama Salma Kikwete akitoa salam za Mwisho
Name:  6.png
Views: 687
Size:  395.4 KBSpika wa Bunge la JMT, Mama Anne Makinda akitoa heshima za Mwisho


Name:  8.png
Views: 684
Size:  316.5 KBMakamu wa Rais Dr. Bilal akitoa salam za pole kwa Mgane wa Marehem
Share on Google Plus

    Blogger Comment