Mgombea ubunge jimbo la Iringa mjini kupitia chama cha Democratic
Party (DP)Bw Robarth Kisininiakizunguka mitaano kuhamasisha wananchi
kufika katika mkutano wake wa uzinduzi wa kampeni za ubunge pamoja na
kunadi sera za chama chake
WAKATI
wagombea wa nafasi za ubunge katika majimbo mbali mbali wa vyama vya
upinzani wakitumia nguvu kubwa ya kujinadi kwa kukodisha magari ya
vipaza sauti mgombea ubunge jimbo la Iringa mjini kupitia chama cha
Democratic Party (DP)Bw Robarth Kisinini amezindua kampeni zake za
ubunge kwa aina ya kipekee baada ya kuzunguka mitaano na msafara wa
Baiskeli mbili zenye vipasa sauti huku moja akiendesha mwenyewe
akihamasisha watu kufika katika mkutano wake .
Mgombea
huyo ambae aliacha ngunzo la aina yake katika mitaa mbali mbali
aliyopita kuhamasisha wananchi kujitokeza kwenye uzinduzi wa
kameni zake jana ,alisema amelazimika kutumia usafiri huo ili
kuwaonyesha wananchi wa jimbo la Iringa mjini kuwa mbunge wanaemtaka
sio mbunge wa mbwembwe na matumizi ya nguvu kubwa katika kampeni zake
bali ni mbunge wa kutumwa kama mwakilishi wa wananchi bungeni.
Kwani
alisema kuwa sababu hasa ya maendeleo ya jimbo hilo kwa miaka
mitano kutoonekana ni kutokana na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo
mchungaji Peter Msigwa (chadema) kutumia muda wake wa miaka mitano
kurudisha gharama zake za kampeni badala ya kuwaletea wananchi wake
maendeleo.
Hivyo
alisema iwapo wagombea ubunge wangefanya kampeni za gharama nafuu kama
zake hali ya kimaendeleo katika jimbo hilo ingeweza kuonekana ndani
ya mwaka mmoja pekee na sio kuja na kauli ya kuwa miaka mitano ya
mbunge bila kuleta maendeleo ilikuwa ni miaka ya kujifunza
kuwawakilisha wananchi.
Bw
Kisinini alisema nguvu kubwa inayotumiwa na chama cha mapinduzi (CCM)
kutaka kupokea jimbo hilo na nguvu kubwa inayotumiwa na aliyekuwa
mbunge wa jimbo hilo Mchungaji Msigwa kutaka kuendelea kuwa mbunge
bila kufanya kazi ,ingeweza kutumika kuleta maendeleo katika jimbo hilo
badala ya vyama hivyo kuvimbishiana misuli kwa kutumia gharama kubwa
ya kampeni.
"
Jimbo la Iringa mjini kwa miaka mitano limeshindwa kabisa kuwa na
maendeleo kutokana na mvutano wa Chadema na CCM hivyo mimi nimeamua
kujitokeza ili kuleta maendeleo ya kweli katika miundo mbinu ,afya
,mazingira na kuona vijana wanakuwa na maisha bora"
Kwani
alisema ubunge wake utakuwa tofauti na aliyekuwa mbunge wa jimbo
hilo mchungaji Msigwa kwani kwa upande wake kampeni zake hazina
gharama kubwa zaidi ya maji ya kunywa katika mikutano na chakula kwa
kijana wake mmoja anaezunguka nae kuhamasisha watu kufika katika
mikutano yao ambayo hata 100,000 kwa muda wote uliobaki haitatumika.
Alisema
wananchi wa jimbo hilo watakuwa wamefanya makosa iwapo
wataendelea kutoa kura zao kwa wale ambao walipata kuwa wabunge wa
jimbo hilo bila kuonyesha kazi waliyoifanya na kuwa njia pekee ya
kufanikiwa katika maendeleo ni kumchagua yeye (Kisinini) kuwa mbunge wa
maendeleo katika jimbo hilo.
Kuhusu
vipaumbele vyake iwapo atakuwa mbunge wa jimbo hilo alisema ni
pamoja na kuboresha huduma za afya kwa kuhakikisha Hospitali ya
wilaya hiyo iliyopo Frelimo inakuwa na madawa na huduma bora zaidi
,pia kuboresha miundo mbinu katika mitaa mbali mbali na kuboresha
sekta ya elimu
MWISHO
Blogger Comment