Profesa Lipumba kuvuliwa Uanachama wa CUF kesho

Wakati  Lipumba  akiwaambia waandishi  wa  habari  jana  kwamba  kadi  yake  ya  uanachama bado  iko  hai  hadi  mwaka  2020,  akimaanisha  kuwa  ataendelea  kuwa  mwanachama  wa  CUF  nje  ya  uongozi,  taarifa  zilizotufikia  zinasema  kuwa  chama  hicho  kinajiandaa  kumfukuza.

 Katika  sehemu  ya  taarifa  iliyotolewa  jana  na Kaimu Mkurugenzi  wa  habari, Uenezi  na  Umma  wa  CUF,Ismai  Jussa,  inasomeka;

 "....Katibu  Mkuu ameagiza  kuitishwa  vikao  vya  dharura  vya  kamati  ya  utendaji  ya  taifa na  Baraza  Kuu  la  Uongozi  la  Taifa  Jumapili, Agosti  9  2015,kujadili  hatua  hiyo  na  kufanya  uamuzi  juu  ya  hatua  muafaka  zinazopaswa  kuchukuliwa  katika  kipindi  hiki."

Mpekuzi  imedokezwa  kuwa  miongni .mwa  uamuzi  unaotarajiwa  kufikiwa  kesho  na  vikao  hivyo  ni  kumfukuza  ndani ya  chama  hicho  Profesa  Lipumba
Share on Google Plus

    Blogger Comment