Ester Bulaya Aipasua CHADEMA Bunda


Aliyekuwa mshindi wa kura za maoni Bunda Mjini wa Chadema, Pius Masururi ametangaza kukihama chama hicho na kujiunga CCM huku mwenyekiti wa jimbo hilo, Samuel Imanani  na wanachama 50 wakiwamo viongozi wakijivua uanachama.

Masururi, aliyepata kura 65 mbele ya wapinzani wake wa karibu, Magembe Makoye (40) na Ester Bulaya (37) katika kura za maoni zilizopigwa Julai 29 mwaka huu, ametangaza uamuzi wake huo jana kupitia kituo cha redio cha Mazingira FM cha mjini Bunda.

Masururi amesema ameamua kukihama chama hicho baada ya kutofurahiswa na kitendo cha Kamati Kuu ya Chadema kupuuza uamuzi wa wanachama kwa kukata jina la aliyeshinda kura za maoni.

Katika jimbo la Bunda Mjini, Chadema imebadilisha matokeo na kumteua mshindi wa tatu, Ester Bulaya kupeperusha bendera ya chama hicho, jambo lililowaudhi baadhi ya makada wake.

Baadhi ya wanachama walioongozwa na mwenyekiti wa jimbo hilo, Samuel Imanani wamesema kitendo cha makao makuu ya Chadema kutengua uamuzi wa kura zao za maoni ni udhalilishaji mkubwa, hivyo hawana budi kukihama chama hicho. 
 
“Tumeamua kuuachia uongozi wa makao makuu uendeshe mambo yote, nasi tusiwe tena wanachama maana hautusikilizwi,” alisema Mashaka Kipili mmoja wa wanachama hao
Share on Google Plus

    Blogger Comment